Sharon, Melon ni mapacha , DNA yaonyesha

Image result for kakamega twins

Ngoja ngoja huumiza matumbo lakini mapacha wa Kakamega wamejawa na furaha mwishowe baada ya matokea ya chembechembe zao kuonyeshwa.

Hatimaye matokeo ya DNA ya wasichana watatu kutoka Kakamega waliotenganishwa kufuatia mkanganyiko uliotokea katika hospitali ya Kakamega General katika wodi ya akina mama kujifungua yametolewa rasmi.

Image result for kakamega twins

Kwa mujibu wa ripoti kwenye matokeo hayo ya Jumamosi, Juni 15, Sharon Mitekwa na Melon Lutenyo ni mapacha na chembechembe zao zinafanana kwa asilimia mia (100%).

Matokeo hayo aidha yalifichua kwamba Rosemary Onyango ni mama ya pacha hao ambao walifanana kama shilingi kwa reale.

Related image

Matokeo pia yamemtenga Bi Onyango kuwa mama wa kibaiolojia wa Mevis Mbaya na 12 kati ya 23 ‘loci’ yalijaribiwa kuonyesha kutofautiana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *