Naibu Rais William Ruto amemkabidhi riziki mpinzani wa gavana John Lonyangapuo ambaye alisemekana kuwa mfupi, mnono, na duara na wala usingejua mbele ama mgongo wake.(Mfupi mnono round).
Wiki chache iliyopita, chiu wa Pokot Magharibi alivuma kwa mtandao baada ya gavana kumkejeli na msemo wa kijana fupi round ambayo iligeuka kuwa fani ya ucheshi.
“Kijana fupi, amenona round, huwezi juatumbo ni wapi na mgongo ni wapi, hana kazi, hana kazi,” alisema gavana Lonyangapuo.
Mpinzani wake Dennis Ruto Kapchok, atapewa kazi nzuri baada ya naibu rais kuwaahidi wakaazi kwamba atmpatia akaz ili akuwe na shughuli nyingi aache kumsumbua gavana Lonyangapuo.
Akiongea kwa Pokot Magharibi ambapo alizindua mradi wa shule mnamo Ijumaa, alisema Mulmwa lazima awe mwangalifu kwa kupuuza miradi ya serikali.
“Mulamwas atapata kazi, lakini anafaa kukoma kuzuia miradi ya serikali. Kazi yake sio ya kuzuia mjengo wa sehemu ya maji taka, hiyo si kazi ni upuzi. Kama anataka kazi atfute moja na nitamsaidia kupata kazi.”