Swali la Richard Mabala kuhusu Rais na Urais limezua mjadala mtandaoni

Kupitia ukurasa wake rasmi wa Twitter Richard Mabala ambaye ni mwandishi maarufu wa vitabu, mwanafasihi, mkereketwa wa elimu ya Tanzania, mhamasishaji wa matumizi ya lugha ya Kiswahili kama lugha rasmi ya kufundishia nchini, mwanasafu kwenye magazeti mbalimbali na mwanaharakati kupitia Asasi binafsi ameulizwa swali kwamba ‘Rais ni taasisi au Urais ni taasisi’

Kufuatia swali hilo watu kibao wamekuja na majibu yao ambayo kila mtu anaona ni sahihi ambapo Richard mwenyewe amechagua lake ambalo ni sahihi zaidi kwake.

Richard Mabala anatambulika kwa vingi hapa Tanzania, kwa wale waliopita elimu ya sekondari basi watakuwa wakimjua kupitia vitabu kama Mabala The Farmer na Hawa the Bus Driver. Wengine watamkumbuka kwa mashairi yake ya Kiingereza yaliyomo kwenye vitabu vya Summons: Poems From Tanzania na Selected Poems

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *