Kadaga awaonya wabunge kabla ya hotuba ya rais Museveni

Image result for museveni public address

Msemaji wa bunge la Uganda Rebecca Kadaga amewaonya wabunge leo dhidi ya kupigia kelele rais Yoweri Kaguta Museveni mbele ya ukumbi wa hali ya taifa ambayo imepangwa tarehe 6 mwezi wa Juni.

Rais Museveni atahotubia wananchi wiki ijayo huku bajeti ya 2019/2020 itatolewa Alhamisi 13, 6, 2019. Kadaga aliangazia hotuba ya rais ya mwaka jana ambayo wabunge walionyesha ukosefu wa nidhamu.

Image result for ugandan mps

“Najua wengine wenu wanapenda kuonyesha wao ni kina nani kwa umma. Kulikuwa na ukosefu wa nidhamu mwaka jana wakati wa hotuba ya rais,” alisema Kadaga.

Kadaga alisema kuwa tabia ya wabunge ilionyesha picha mbaya ya nchi.

Image result for ugandan mps

“Kwa kweli, spika wenzangu wa kanda zetu walishtuka kuona watu wakimdhalilisha rais. Ukweli kuna uhuru wa kujieleza lakini ni tofouti na heshima,” aliongezea.

Aliwaonya viongozi wa upinzani na wale wa kujisimamia kukoma kutupia rais matusi ambayo inaonyesha taswira mbaya ya nchi.

Rais Museveni alisema juzi akiwa Hoima kwamba watu wanachukulia uhuru wa kujieleza vibaya na kumtusi wanapotaka kwa maredio na televisheni.

“Kuna uhuru mwingi Uganda mpaka watu wananitusi kwenye maredio na mitandao ya kijamii,” Museveni alisema.

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *