Hii ndiyo faida aliyopata Mwanadada aliyevamia uwanja fainali ya UCL, Spurs Vs Liverpool

Wahenga wanasema Mungu huonesha njiia mahali ambapo hapana njia. Jumamosi wakati mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya timu mbili kutoka nchini England za Tottenham Hotspur na Liverpool ukiendelea aliibuka mwanadada Kinsey_Wolanski kutoka jukwaani na kuvamia uwanja akiwa amevalia nguo mithili ya zile za kuogelea, lengo likiwa ni kutangaza tovuti ya mchumba wake.
Kabla ya Mwanamitindo huyo wa Kimarekani kuvamia uwanja, alikuwa na wafuasi 230,000 kwenye Instagram lakini mpaka saa 12 baada ya tukio lile tayari alishavuna zaidi ya wafuasi milioni moja.
Licha ya Mwanadada huyo kuelezwa kuwa atakumbana na rungu la adhabu, lakini anaonekana kutokujali chochote ili mradi dhamira yake imetimia.

Akielezea sababu hasa iliyomfanya kuvamia uwanja, amesema: “Maisha ni kwaajili ya kuishi, fanya mambo makubwa ambayo yataacha kumbukumbu milele.”
Tukio hilo limeongeza thamani kwa website ya mchumba wake na kukadiriwa kufikia thaani ya karibu dola milioni nne
Baada ya tukio hilo mchumba aliandika kwenye Instagrama yake hivi: “Nasubiri kwa hamu siku ya ndoa yetu.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *