Mashine hii ya KI-IVORY COAST ndiyo mrithi wa Juuko Simba

Huku purukushani za usajili zikiwa zimeanza kupamba moto kwa vilabu vya soka hapa nchini hususan Yanga na Simba, Simba wamehusishwa na usajili wa beki kitasa Muivory Coast Ange Bares ayekipiga katika klabu ya Es Metlaoui ya Tunisia.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 32 ameingia kwenye mipango ya Simba ikiwa ni moja ya mapendekezo ambayo Kocha Patrick Aussems aliyataka ya kuhitaji beki mmoja a kati mwenye uwezomkubwa zaidi.

Vyanzo mbalimbli vinaonesha kuwa beki huyo aliwahi kuvichezea vilabu vya Horoya Athletic ya Guinea na Asec Mimosas ya Ivory Coast.

Imeelzwa kuwa wakala wake Patrick Gakumba ambaye amemalizana na bodi ya wakurungezi ya klabu ya Simba kumleta beki huyo ili achukue nafasi ya Juuko Murshid anayeondoka Simba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *