Mambo makubwa sita ya kufahamu Liverpool ikiitandika Spurs 2-0 Fainali ya UEFA

Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu wa 2018/19 umemealizika rasmi usiku wa kuamkia leo ambapo miamba miwili ya England Liverpool na Tottenham walikuwa wakipambana na Liverpool hatimaye Liverpool kunyakuwa ndoo kwa ushindi wa mabao 2-0.

Mohammed Salah ambaye aliumia katika fainali ya msimu uliopita dhidi ya Real Madrid alianza kuifungia Liverpool mapema dakika ya pili kwa penati baada ya Moussa Sissoko kuunawa mpira ndani ya eneo la penati na Divock Origi akaifungia Liverpool bao la pili dakika ya 87.

  • Hii ni mara ya sita Liverpool kushinda kolmbe la UEFA, mara mbili zaidi ya timu inayomfuatia nchini England ambayo ni Manchester United (mara tatu).
  • Klopp anakuwa meneja wa wanne wa Liverpool kushinda kombe la Ulaya baada ya Bob Paisley, Joe Fagan na Rafael Benitez.
  • Klopp ni meneja wa tano wa Kijerumani kushinda Kombe la Ulaya, baada ya Dettmar Cramer, Jupp Heynckes, Ottmar Hitzfeld na Undo Lattek lakini ni wa pili pekee kutoka Ujerumani kushinda na timu ambayo si ya Ujerumani (Heynckes akiwa na Real Madrid).

  • Pochettino amepoteza mechi zake zote kubwa za fainali akiwa kama kocha wa Tottenham, pia akipoteza katika fainali ya kombe la Ligi dhidi ya Chelsea mwaka 2015.
  • Hii ni mara ya kwanza kabisa kwa Tottenham kufika fainali ya Michuano ya Ulaya, na kufanya kufikisha idadi ya timu nane za Kiingereza kuwahi kufanya hivyo. Wanafanya idadi ya timu sita zilizoingia fainali kwa mara ya kwanza kupoteza (Chelsea 2008, Arsenal 2006, Monaco 2004, Bayer Leverkusen 2002 na Valencia 2000).
  • Liverpool (35.4%) imekuwa timu ya kwanza kushinda fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya licha kuwa na umiliki mdogo wa mchezo dhidi ya wapinzani wao. Mara ya mwisho kutokea hivyo ilikuwa mwaka 2010 wakati Inter Milan ya Jose Mourinho aliposhinda dhidi ya Bayern Munich mwaka 2010.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *