Homa ya Dengue: Wanaohamasisha matumizi ya maji ya mipapai kuchukuliwa hatua kali

Wizara ya Afya Maendeleo Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Tanzania imesema kuwa itaanza kuchukua hatuakali dhidi ya watu wanaojirekodi na kusambaza klipu zinazosema watu wanywe maji ya mipapai au kupaka mafuta ya nazi ili kujitibu na homa ya Dengue

Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam na Naibu Waziri wa Wizara hiyo,  Dkt. Faustine Ndugulile alipotembelea eneo la Jangwani ambalo ni moja ya mazalia makubwa ya mbu jijini humo

“Tunasema ugonjwa huu hauna tiba hivyo mtu yeyote anayeona ana dalili hizo ni kufika kituo cha afya”.  Alisema

Viongozi wa Wizara hiyo Ummy Mwalimu, Faustine Ndugulile pamoja na Viongozi wa Mkoa wa Dar es salaam leo wametembelea eneo la Jangwani Dar es salaam ikiwa ni sehemu ya mikakati ya kudhibiti ugonjwa wa homa ya Dengue nchini.

Hatua zilizokubaliwa kuchukuliwa na uongozi wa Wizara ya Afya na wa Mkoa wa Dar es Salaam ili kudhibiti homa ya Dengue ni kunyunyizia dawa za kuua mazalia ya mbu na kutoa vipimo vya ugonjwa wa Dengue bure kwenye vituo na hospitali za umma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *