Msanii wa Bongo Fleva Naseeb Abdul ama Diamond Platnumz anatarajiwa kupiga show jijini Nairobi katika uwanja wa mpira wa Moi Kasarani siku ya tarehe 8 ya mwezi huu katika tamasha la ‘Tomorrow’s Leaders Festival’lilioandaliwa na kundi la muziki la Morgan Heritage la nchini Jamaica.
kupitia akaunti yake ya instagram Diamond Platnumz alithibitisha juu ya kushiriki tamasha hilo kwa kupost kipande cha video kwaajili ya promo.
View this post on Instagram
‘Tomorrow’s Leaders Festival’ ni tamasha la hisani liliLondaliwa na kundi la Morgan Heritage ili kuchangisha fedha za kuendeleza program ya Uongozi iliyoasisiwa na kundi hilo barani Afrika na nchini Jamaica.
Diamond kwa sasa anafanya vizuri na hit song ya Inama aliyomshirikisha Fally Ipupa toka nchini Congo , Diamond Platnumz pia ana collabo lililofanya vizuri na kundi la Morgan Heritage liitwalo haleluyah nae alishirikishwa pia kwenye wimbo wa ‘Africa Jamaica’ wa kundi hilo.
Mbali na Diamond Platnumz wasanii wengine ni mwanadada Alain kutoka Jamaica,Wyre toka kenya, Yemi Alade from Naija, Jose Chameleone from Uganda na wenyewe Morgan Hertage na wasanii wengine kibao.
View this post on Instagram
KUHUSU MOI KASARANI STADIUM
Unajulikana kama Uwanja wa Kimataifa wa Michezo wa Moi na shughuli mbalimbali hufanyika kwenye uwanja huu ambao hubeba takribani watu 60000 uko nje kidogo ya jiji la Nairobi, Kenya.
Ulijengwa mwaka 1987 na ulifadhiliwa na serikali ya China kwa ajili ya All-Africa Game iliyofanyika mjini Nairobi. Unatumika kwa sasa haswa kwa mechi za kandanda, Timu ya Kitaifa ya Kenya huchezea mechi zake nyingi za nyumbani hapa. Kando na uga wa kandanda, kuna pia ukumbi unaobeba watu 5,000 wa Gymnasium na ukumbi wa kuogelea kama sehemu ya Uwanja wa Kimataifa wa Michezo wa Moi.
Katika nyanja za burudani ya muziki uwanja huu unahistoria ya kufanyika Sherehe za mwaka wa 2009 za MTV Africa Music Awards zilizoandaliwa na kituo cha luninga cha MTV.