Tunda Man: Hata Nikilipwa Milioni 100 Siwezi Kuitungia Yanga Wimbo.

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva Tundaman amesema hata alipwe milioni 100  za kitanzania hawawezi kuitungia wimbo klabu ya soka ya Yanga.

Tundaman anafahamika kuwa mnazi mkubwa wa Klabu ya wanamsimbazi na anatamba na wimbo maaufu wa naipenda Simba shabiki wa damu inayopendwa sana na mashabiki wa klabu hiyo uliotayarishwa na producer Mensen Selekta.

Akizungumza na Dizzimonline mara baada ya kushuhudia tuzo  za MoSimba Awards amesema kuwa alipotunga wimbo huo wa Simba  hakumshirikisha kiongozi yoyote wa Simba bali ni mapenzi yake kwa Klabu hiyo ndo yaliyomsukuma.

Na alipoulizwa juu ya kuitungia Klabu ya Yanga wimbo amesema hata alipwe milioni 100 hatoweza  kuitungia Klabu hiyo ya wanajangwani.

Cheki interview kamili hapa chini:

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *