Serikali yamwaga pesa kwa vijana

Serikali yatoa mkopo wa bilioni 2.57 kwa vijana 978 wa mkoa wa Dodoma ili kuhakikisha vijana wananufaika  na serikali kuhamia jijini Dodoma.

Hayo yamesemwa bungeni na Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde

Hatua zingine zilizochukuliwa ni pamoja na kuwapatia mafunzo ya kuandaa kitalu nyumba (green house) kwa vijana 800 pamoja na kurasimisha ajira zisizo rasmi.

Mbali na hilo, hatua zingine zilizochukuliwa ni pamoja na kuwapatia vitambulisho vya ujasiliamali na kuwahamasisha kuunda makampuni na tayari makampuni 12 yameshaundwa.

Kwa sasa Bunge linaendelea Bungeni jijini Dodoma ambapo Mawaziri mbalimbali wameendelea kuwasilisha makadirio yao ya bajeti kwa mwaka wa fedha 2019/2020

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *