Mwanamke aliyejichana tumbo na kumtoa mtoto azua gumzo

Sakata la mwanamke Joyce Kalinda (30) kudaiwa kujichana tumbo na kitu chenye ncha kali na kumtoa mtoto akiwa ndani ya tumbo limeleta gunzo kwa wakazi wa kata ya Kirando wilayani Nkasi mkoani Rukwa.

Tukio hilo ambalo ni la aina yake lilizua taharuki kubwa kwa wananchi hao ambao walilazimika kufika katika kituo hicho cha afya ili kuthibitisha taarifa hizo kama zina ukweli kwa mwanamke huyo kujifanyia upasuaji wa tumbo na kumtoa mtoto tumboni mwake.

Mganga Mkuu wa Wilaya ya Nkasa, Dk. Hashi Mvogoro akizungumzia tukio hilo alisema bado uchunguzi unafanyika ili kujua ukweli wa jambo hilo.

Alisema uchunguzi huo ni pamoja na kubaini kama mwanamke huyo alijifanyia upasuaji mwenyewe na kutoa mtoto tumboni au kuna mtu mwingine alifanya hivyo.

Ilidaiwa kuwa majira ya saa 9 alfajiri kuamkia jana mwanamke huyo alifika katika kituo cha afya cha Kirando na kuanza kupiga kelele na kumtaka muuguzi aliyekuwa zamu ampatie huduma ili ajifungue.

Kutokana na kuwepo kwa wagonjwa wengine kituoni hapo muuguzi alimshauri mjamzito huyo kusubiri kidogo na kwenda kutoa huduma kwa mgonjwa mwingine.

Hata hivyo, baada ya kurejea hakumkuta na muuguzi huyo alikwenda kwa mlinzi na kumuuliza na kumjulisha mwanamke huyo ametoka nje ya kituo bila kuaga anakokwenda.

Kwa mujibu wa Dk. Mvogogo alieleza kuwa ilipofika saa 11 alfajiri mjamzito huyo alirudishwa kituoni hapo akiwa amepasuka sehemu za tumbo huku waliomfikisha hospitali hapo wakiwa na mtoto mchanga.

“Alipofika kituoni hapo aliwekewa dripu tatu za damu ili kuokoa maisha yake kwani alipoteza damu nyingi na mtoto alipatiwa matibabu na wanaendelea vizuri,” alisema Dk. Mvogogo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *