MLINZI WA ZAMANI WA RAIS PAUL KAGAME AUAWA AFRIKA KUSINI

Gari linalodaiwa kuwa ndilo alikuameabiri Camir na kumiminiwa risasi.Capetown

Camir Nkurunziza aliyewahi kuwa mlinzi katika kikosi cha kumlinda  raisi Paul Kageme wa Rwanda ameuwawa siku ya jana Cape Town nchini Afrika ya kusini.

Taarifa zinadai kuwa Camir aliuwawa kwa kupigwa risasi, hi inakuja baada ya wiki moja tangu raisi Paul Kagame kuhudhuria kuapishwa kwa rais Cyril Ramophosa wa Afrika Kusini.

Mauaji haya yamefanyika ikiwa ni miaka 5 baada ya kuuawa kwa aliyekuwa Afisa Mwandamizi wa Usalama wa Taifa wa Rwanda, Kanali Patrick Karegeya

Nkurunziza anakumbukwa kwa kuanzisha kampeni ya kupinga Rais Kagame kuongozewa muhula wa 3 na mara kadhaa alionekana amevalia bango linalopinga kumuongezea muhula wa tatu Paul Kagame lililokuwa likisomeka ‘No third term for Kagame Article 101’

Camir Nkurunziza enzi za uhai wake.

Camir ni kaka wa sajini Innocent Karisa ambae amekamatwa na kushitakiwa mashitaka ya ugaidi nchini Rwanda na alikamatwa nchini Uganda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *