Juma Nature:Pombe Haijawahi Niathiri kwenye Muziki/Aeleza Kutopanda Jukwaani Wasafi Festival Morogoro.

Msanii wa bongo fleva Juma Nature amesema kuwa pombe haijawahi kumuthiri katika muziki wake na  ameanza kunywa pombe  tokea ananza muziki.

‘Toka naanza gemu napiga mitungi mpaka unaniona hivi ,show zangu zote nazopiga na unazisifia nimepiga munde na watu wanaruka’

Miaka ya hivi karibuni kulikua na minong’ono kuwa ameshuka kimuziki  kutokana na kutumia muda mwingi kwenye pombe.

Mwishoni mwa mwaka jana kwenye show ya Wasafi Festival iliyofanyika mkoani Morogoro  alishindwa kupanda jukwaani kwa wakati na ikahisiwa kuwa alikua amelewa pombe.

Akiongea na kipindi cha Block 89 cha Wasafi Fm ,Juma Nature amesema kuwa muda wa kupanda jukwaani kwake ndo ulikua changamoto kwani alitakiwa kupanda Jukwaani saa 11:00 alfajiri muda ambao anadai  hakukuwa na vibe kutoka kwa mashabiki. Cheki interview yote kwenye link hapa chini.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *