Dula Makabila azungumzia kumtumia Sholo Mwamba Feki kwenye Dua.

Mkali wa muziki wa kisingeli nchini Tanzania Dulla Makabila amezungumzia ishu  yake ya kumtumia shollo Mwamba feki katika video yake mpya ya ‘Dua’

Katika wimbo huo wa kuna mstari unaomdisi Sholo Mwamba kwa kumtaka aache kuimba amlindie mbwa wake nyumbani na ndani  ya video hiyo ametumika jamaa mwenye kufanana na Sholo Mwamba akiwa ameshika mbwa. Hali iliyozua sintofahamu kwa mashabiki wa muziki huo.

Kwa muda  mrefu kulisemekana kuwa na  bifu baina ya hao wawili. Na hivi karibuni alipohojiwa na kipindi cha Refresh cha Wasafi Tv, Dulla Makabila amedai kuwa hana shida yoyote na Sholo Mwamba na alimtaka kumtumia kwenye video hiyo ila aliona kutakuwa na ugumu kumtumia.

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *