Aliyefufua kaburi la baba yake aendeleza sinema

 

Maajabu yazidi kujitokeza katika sakata la kijana, Joseph Salum (28) ambaye alifukua kaburi la baba yake kwa ajili ya kutaka kuchukua blanketi  ameendelea kufanya vituko kwa kuwakimbia askari akiwa eneo la mahakama.

Salum ambaye ni wa mkazi wa kijiji cha cha Makiwaru Ngalitati katika Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro anatuhumiwa kufukua kaburi la baba yake bila kuwa na kibali wiki iliyopita.

Ilielezwa kuwa kabla ya kuwatoroka askari hao, alifikishwa katika mahakama ya Wilaya ya Siha kwa ajili ya kusomewa shtaka la kufufua kaburi la baba yake aliyezikwa tangu mwaka 2016 bila kuwa na kibali kwa kudai lengo lake achukue blanketi ajikinge na baridi.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilmanjaro, Hamis Issah, akizungumzia tukio hilo alisema baada ya kutoroka alikimbilia katika kaburi hilo ambalo alilifukua awali kwa ajili ya kutafuta blanketi .

“Mtuhumiwa alifikishwa mahakamani na katika hali iliyozua taharuki alitimka mbio akiwa mahakamani hapo na hakuweza kupatikana kwa siku hiyo na siku ya pili alikamatwa na wananchi kwa kushirikiana na polisi akiwa eneo la kaburi hilo alilolifua kwani hakuamini kama ndani ya kaburi hilo hakuna blanketi la baba yake alilozikwa nalo tulimkamata na kumfikisha polisi” alisema

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *