Watakao Kamatwa na Mifuko ya Plastiki Kufungiwa Uwanja wa CCM.

Jeshi la Polisi Mkoani Arusha limesema kuwa litalazimika kuwafungia watakao kutwa na mifuko ya plasitiki uwanja wa mpira wa Sheikh Amri Abeid endapo mahabusu zote zitakuwa zimejaa.

Watuhumiwa wote watahifadhiwa uwanjani hapo hadi pale watakapofikishwa Mahakamani

Kuanzia Juni mosi, 2019, itakuwa ni marufuku kutengeneza, kuingiza, kuuza na kutumia mifuko ya plastiki kwa ajili ya kubebea bidhaa na matumizi yake yatakoma ifikapo Mei 31, 2019 na tayari serikali imeshetoa tamko kuwa haitoongeza muda.

SHEIKH AMRI ABEID STADIUM.

Uwanja huo uko kilomita chache kutoka kituo kikuuu cha polisi jijini Arusha na mahakama maarufu ya Kaloleni.

Uwanja huo wa michezo upo katikati ya mji wa Arusha, kiwanja namba 153 kitalu 21 katika eneo la Kaloleni, ukiwa na ukubwa wa ekari 6.53 na unaweza kuingiza kwa wakati mmoja watu kati ya 16,000 na 20,000, ujenzi wake ukiwa umefanyika kati ya mwaka 1976 na 1977, kwa nguvu za wananchi wa Arusha na serikali

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *