Nandy aelezea jinsi Willy Paul ni mwoga

Image result for willy paul and nandy

Msanii wa Tanzania Faustina Charles Mfinanga almaarufu Nandy amefunguka na kuyaelezea matukio yaliyotokea wakati wakirekodi Hallelujah na msanii wa injili Willy Paul.

Kupitia video aliyoiweka Willy Paul kwenye mtandao wa Instagram mnamo Mei 2, anaonekana mwenye kuaibika alipoguzwa kwenye mabega na mwanadada huyo wa Tanzania.

Image result for willy paul and nandy

Willy Paul aliweka video ile na kufuatia maelezo; “”Bikira mvulana, wataje wanaume wote wenye haya … @officialnandy amenifanya kujisikia mwoga wakati yeye alinigusa kwanza kwa video hii … Mimi sina mazoea ya aina hii ya filamu! Tazama na uacha maoni.”

Katika mahojiano ya kipekee na Word with SDE, mwimbaji wa Tanzania alielezea kwa nini Willy Paul alikuwa na mwonekano wa uoga kwenye harakati za kutengeneza video ya Hallelujah.

“Willy Paul ni mwoga. Aliblush kwa vile anajitambulisha kama gospel artiste.”

Pia aliongezea kuangazia tuhuma zilizotolewa kwa wimbo wa Hallelujah kama mziki wa injili ilhali ilisheheni vipengee ambavyo haviruhusiwi kwa mziki wa kuabudu Mungu.

Related image

“Hallelujah inatumika kwa maana nyingi. Tuylivyomaanisha sisi ni kama unavyoweza kuona kitu kizuri useme Hallelujah, kumaanisha Mungu kaumba”

Willy Paul kwa upande wake, amedhalilisha mziki wa injili na kujitwika kwa ulingo wa burudani za dunia kama alivyoonekana katika uwepo wake paleHouston Marekani.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *