Nataka kufanya usajili ambao utakuwa na tija-Zahera kuhusu usajili wa Ndemla

Kufuatia tetesi nyingi kuhusu usajili wa kiungo wa klabu ya Simba Said Ndemla kuhusishwa kujiunga na klabu ya Yanga , Kocha Mkuu wa Klabu ya Yanga, Mwinyi Zahera ameweka wazi kuwa kwa sasa hana mpango wa kumsajili kiungo kiungo huyo ambapo amesema kwa sasa anaagalia wachezaji watakaisaidia timu yake zaidi.

Zahera amesema kuwa mpango wake ni kuhakikisha anakuwa na kikosi imara na bora ambacho kitakuwa na ushindani msimu ujao kutokana na aina ya wachezaji ambao amewapendekeza kwaajili ya kusajiliwa.

“Sina mpango wa kumsajili Said Ndemla, simjui huyo mchezaji na hayupo kabisa kwenye hesabu zangu.

“Nataka kufanya usajili ambao utakuwa na tija hivyo mashabiki wa Yanga watulie wasiwe na presha kila kitu kitakuwa sawa,” Zahera amenukuliwa na mtandao wa Saleh Jembe

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *