Mpenzi wa Rayvanny aweka wazi tarehe ya harusi yao

Image result for rayvanny and fahvanny

Mpenzi wa Rayvanny wa muda mrefu, Fahyma amethibitisha harusi yao imewekwa Julai tarehe 7, 2019.

Mama mtoto wa Rayvanny mtoto aliweka picha yake kwenye mtandao wa Instagram akiwa amevalia vazi la harusi na maelezo ya maneno;

“Hifadhi tarehe 7/7/2019.”

Image result for rayvanny and fahvanny

Inaonekana Jumapili Julai 7, 2019 ni tarehe mwanamtindo huyo atafunga pingu za maisha na mpenzi wake wa muda mrefu, msanii Rayvanny.

Ni mwaka moja na nusu sasa tangu Rayvanny na Fahvanny wamkaribishe kifungua mimba wao na wameonyesha kuwa na nia wa kwenda mbali pamoja.

Image result for rayvanny and fahvanny

Rayvanny aliweka wazi kuwa anamheshimu mpenzi wake kwa kile alisema uhusiano wao ni wa ‘kikonki’ na imara na watapanga siku ya harusi.

Rayvanny anajulikana sana kwenye kikundi cha WCB Wasafi kuwa mtu wa familia na kumtunza mpenzi wake. Picha anazozionyesha kwenye mtandao inazungumza mengi na kuonyesha ukaribu wake na familia yake.

 

View this post on Instagram

 

KING @jaydanvanny

A post shared by C H U M A (@rayvanny) on

Kumaanisha tunangojea harusi?

Rayvanny kwa upande wake hajazungumzia hili lakini pindi tu anapoamua kutoa maelezo tutakuletea habari hiyo moja kwa moja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *