Mchina mbaroni kwa kukamatwa na mashine feki 1000

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekamata mashine haramu 1,006 za michezo ya kubahatisha zilzokuwa zinailikiwa na raia wa Kichina ambazo zingeingizwa sokoni serikali ingekosa kodi ya Sh billion 1.2.

Meneja Msadizi Madeni TRA Ilala, Stephen Kauzeni, alisema Mei 23 mwaka huu raia wema waliwapatiwa taarifa ya kuwepo kwa mashine kwenye maghala mawili katika eneo la Mikocheni na Kilongani.

Alisema walipofuatilia kwa kushirikiana na vyombo vya usalama walifika katika eneo la Mikocheni walikuta eneo hilo hutumika kutengeneza na kuhifadhia mashine hizo.

Kauzeni alisema idadi ya mashine hizo zilikuwa zinaingizwa sokoni na kwamba ingeisababishia serikali kupoteza kodi ya Sh bilioni 1.2 kwa kila mwaka ingawa wamefanikiwa kuzizuia.

Alisema taarifa iliyopo kuna mashine nyingine ambazo tayari zimeshaingia sokoni ambazo kwa sasa wanaendelea kuzifutilia kwa ukarabu na taarifa yake itatolewa kwa baadaye.

Kauzeni alisema mmilki wa mashine hizo ni raia wa nchini China ambaye anaendelea kuhojiwa na vyombo vya usalama na ameshindwa kutoa nyaraka za kuingiza mashine hizo na wao wanafahamu mashine hizo zimetoka nje ya nchi.

Alisema katika maelezo ya mchina huyo ametaja kushirikiana na raia wa Tanzania ambaye yupo mkoani Arusha katika biashara hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *