Ligi Kuu Bara imemalizika rasmi leo, zilizoshuka, zitakazocheza play Off hizi hapa

Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo imefika ukingoni rasmi ambapo Simba wamekabidhiwa rasmi ubingwa wa baada ya kujikusanyia jumla ya alama 93 huku timu nyingine zikiteremka rasmi daraja

Timu ambazo mpaka sasa zimeshuka daraja moja kwa moja ni African Lyon  mwenye pointi 23 na Kagera Sugar yenye pointi 44.

Kwa mujibu wa takwimu kutoka Bodi ya Ligi kabla ya michezo GD ya Stand United ilikuwa -9 na GD ya Kagera Sugar ilikuwa -11 matokeo ya Leo

FT’ JKT Tanzania 2-0 Stand United
FT’ Mbao FC 1-1 Kagera Sugar

Maana yake Stand United imebaki na pointi zake 44 na GD ya -11 na Kagera Sugar imekuwa na Pointi 44 na GD ya -11

Kwa maana hiyo GD zinafanana wote -11 kinachofuata ni Head to Head mechi ya kwanza ya Stand na Kagera ilifanyika Shinyanga na Matokeo yalikuwa 1-1 na mechi ya pili ilifanyika Kagera matokeo Stand ilishinda kwa magoli 3-1

Maana yake Stand anakuwa na Faida kwenye Head to Head. Na kwa mjibu wa takwimu hizo African Lyon na Kagera Sugar wameshuka moja kwa moja na Stand United na Mwadui FC zinacheza Play Off.

Mwadui FC imemaliza ikiwa nafasi ya 17 hivyo nayo itacheza play off kama Kagera Sugar.

Matokeo ya leo kiujumla ni haya hapa:

FT: Coastal Union 0-0 Singida United.

FT: Mbeya City 0-0 Biashara United.

FT: Mtibwa Sugar 0-0 Simba SC.

FT: Ruvu Shooting 1-0 Alliance FC (Fully Zullu Maganga 25’ p) .

FT: JKT Tanzania 2-0 Stand United (Samweli Kamuntu 51’, Najimu Maguli 73’).

FT: Ndanda SC 1-3 Mwadui FC (Kigi Makasi : Ottu Joseph 39’, 41’, Salim Aiyee 61’)

FT: Yanga SC 0-2 Azam FC (Daniel Amoah 45’+2, Mudathir Yahya 50’).

FT: Mbao FC 1-1 Kagera Sugar (Hebert Lukindo 60’ : Ally Ramadhan 20’).

FT: Tanzania Prisons 3-1 Lipuli FC (Benjamini Asukile 29’, Adam Adam 48’, 85’ : Seif Rashid 46’).

FT: African Lyon 0-2 KMC FC (Cliff Buyoya 21’, 17’)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *