Harry Kane yuko tayari kuwavaa Liverpool fainali UCL

Nahodha wa Tottenham na Timu ya Taifa ya England Harry Kane amethbitisha kupona majeraha yake na sasa yuko tayari kuwavaa Majogoo wa Jiji England, Liverpool FC kwenye mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya utakaofanyika Juni 1, 2019 katika Uwanja wa Wanda Metropolitano kwenye jiji la Madrid nchini Uhispania.

Mshambulizi huyo hatari alikuwa nje ya dimba akiuguza majeraha yake ya goti la mguu wa kushoto aliyopata wakati wa mchezo wa nusu fainali ya kwanza ya UEFA dhidi ya Manchester City Aprili 9 baada ya kugongana na Fabian Delph.

Awali Meneja wa Spurs Mauricio Pochettino alidhihirisha hofu yake ya kumkosa mshambulizi huyo katika kuelekea mechi zote za kumaliza msimu huu kutokana na taarifa za awali za tatizo hilo.

“Najisikia vizuri. Kumekuwa hamna shida yoyote mpaka sasa,” amesema Kane. “Taratibu nilianza kujihisi kupona mwishoni mwa wiki iliyopita na kwa sasa nadhani niko imara zaidi.”

“Kwa sasa uamuzi wa ama kunichezesha au kutonichezesha nauacha kwa meneja wangu. Lakini mpaka sasa nipo fiti kabisa.

Mpaka kufikia sasa msimu huu, Kane ameifungia Spurs magoli 24 kwenye michuano yote licha ya kukaa nje kwa takribani wiki sita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *