Tetesi: Hii hapa mpya kuhusu Kahata kutua Simba

Hivi karibuni kumekuwa na taarifa mbalimbali kuhusu kiungo mahiri wa Gor Mahia Francis Kahata kutua kunako klabu ya Wekundu wa Msimbazi, Simba Sports Club

Sasa uongozi wa Simba umesema hauna mipango ya kumsajili mchezaji Francis Kahata anayekipiga katika timu ya Gor Mahia FC ya Kenya.

Ofisa Mtendaji wa Simba, Crescentius Magori ameibuka na kusema kuwa hawana mpango wa kumsajili mchezaji huyo kwa sasa.

Licha ya kukanusha kutaka saini yake, Magori amesema ni kweli ameshamaliza mkataba na Gor Mahia na baada ya msimu huu Kahata atakuwa ni mchezaji huru.

“Sisi hatujafanya mazungumzo na Kahata mpaka sasa.

“Hakuna ukweli juu ya taarifa za kuwa tutamsajili.

“Ni kweli ameshamaliza mkataba na Gor Mahia lakini tusubiri mambo yakiwa tayari ripoti ya usajili wetu itafanyiwa kazi.”

Tetesi za usajili wa Kahata kutua Simba zimeanza muda mrefu tangu kuelekea msimu huu unaomalizika Jumanne ya wiki hii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *