Okwi amewaaga mashabiki wa Simba? soma alichokiandika hapa

‘Baibai’ ni neo ambalo mara zote limekuwa likiacha huzuni kila sehemu ambapo mtu amekuwepo kwenye kipindi fulani na kisha kuondoka huku akiwaaga wenzake kwa neno hilo

MSHAMBULIAJI wa Simba, Emmanuel Okwi, kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika maneno ambayo yana viashiria kwamba anaaga hivi.

Bado haijajulikana kwamba anawaanga mashabiki wa Simba ama la kufuatia kutoanisha dhahiri kwamba mrengo wa meno hayo ni nini haswa.

Okwi, ametupia picha yenye maneno yaliyoonyesha kwamba ni kama anawaaga hivi mahabiki zake.

“Goodbye is the saddest word,” (kwa heri ni neno ambalo lina maumivu) ameandika Okwi.

Tangu kutua Simba, Okwi amekuwa ni kipenzi kikubwa cha mashabiki wa Simba kutokana na kuwapa furaha mara zote wnapohitaji.

Mara kadhaa ameondoka klabuni hapo kutafuta maisha sehemu nyingine lakini baada ya muda hurejea tena klabuni hapo, hali inayosababisha mashabiki wa timu hiyo kuwa na mapenzi makubwa naye.

Msimu uliopita wa 2017/18 Okwi, aliibuka mfungaji bora baada ya kufunga mabao 20 na msimu huu mpaka sasa ana mabao 15.

Mpaka sasa uongozi wa Simba haujawa tayari kuzungumzia suala hilo ambalo limezua taharuki kubwa kwa mashabiki wa Simba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *