Kingue Mpondo, Chirwa waidindia AZAM FC,

Inaelezwa kuwaa Kiungo Mcameroon wa Azam FC, Steven Kingue Mpondo ni kama amegomea mkataba mpya ndani ya klabu yake ya Azam FC baada ya kukataa kusaini huku mkataba wake wa awali ukiwa bado haujaisha.

Mchezaji mwingine ambaye pia ameonekana kukataa kuongeza kandarasi mpya ni Mzambia Obrey Cholla Chirwa ikielezwa kuwa bado anasoma upepo kwanza.

Mratibu wa Azam FC, Philip Alando amesema kuwa, hadi sasa kiungo Kingue Mpondo bado hajaongeza mkataba wowote ndani ya klabu hiyo kwa kuwa amehitaji asubiriwe hadi msimu utakaopoisha.

“Tayari tumeshawaongeza mikataba baadhi ya wachezaji wetu akiwemo Donald Ngoma, Bruce Kangwa, Yacub Mohamed na Abdallah Kheri lakini wengine akiwemo Chirwa na Kingue wamataka wasifanye mazungumzo ya kuongeza mkataba hadi ligi itakapoisha, hivyo ligi ikiisha ndio tutaanza kufanya nae

“Kingu amekataa kusaini mkataba hadi ligi itakapofikia ukingoni hivyo tunasubiria ligi itakapoisha ndio tuweze kufanya nae mazungumzo.

“Mikataba ya wachezaji wa Azam ni tofauti na timu nyingine kuna wengine wanamaliza kabla ya msimu kuisha ndio maana mwisho wa msimu hawawi wengi wanaomaliza mikataba,” alisema Alando ambaye ni mchezaji wa zamani wa Kagera Sugar.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *