Kesi ya Shamimu upelelezi haujakamilika

Image result for shamim mwasha

UPANDE wa mashtaka katika kesi ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya Heroin Hydrochloride inayomkabili mmiliki wa Blog 8020 Fashion, Shamim Mwasha (41) na mumewe, Abdul Nsembo(45) umedai upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.
Wakili wa Serikali, Wankyo Simon alieleza hayo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi, Kelvin Mhina, ambapo alidai shauri hilo lilikuja kwa ajili ya kutajwa lakini upelelezi haujakamilika na kuiomba Mahakam kupanga tarehe nyingine.

Image result for shamim mwasha
Baada ya kutoa maelezo hayo, Wakili wa utetezi, Charles Kisoka akishirikiana na Hajra Mungula walidai shauri hilo halina dhamana na kuomba upande wa mashtaka kuharakisha upelelezi.
Wakili Wankyo alieleza amesikia kilichozunguzwa na upande wa utetezi, hivyo watawahimiza wenzao wa upelelezi wafanye haraka na tarehe ijayo wataeleza upelelezi ulipofikia.

Baada ya maelezo hayo, Hakimu Mhina aliahirisha kesi hiyo hadi Juni 10 mwaka huu, washitakiwa wamerudishwa rumande kwa sababu kesi yao haina dhamana. Washtakiwa hao ambao ni wakazi wa Mbezi Beach, wanatuhumiwa kwa shtaka moja la kusafirisha dawa za kulevya.
Shamim na mumewe wanatuhumiwa kusafirisha dawa hizo za kulevya, Mei 1 mwaka huu wakiwa eneo la Mbezi Beach, Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam kinyume na sheria ya uhujumu uchumi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *