Breaking news: Nyalandu akamatwa na TAKUKURU Singida

Aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini Lazaro Nyalandu amekamatwa na Taasisi ya Kupambana na Kuzui Rushwa (Takukuru) akiwa anasimamia uchaguzi wa kata wa CHADEMA mkoani Singida, Kamanda wa Polisi mkoani Singida Sweetbert Njewike amethibitisha.

Mkurugenzi wa Itikadi na Uenezi wa Chadema John Mrema pia amethibitisha taarifa hizo.
Nyalandu ambaye amewahi kuwa mwanachama wa CCM, alijivua uanachama wa chama hicho Oktoba 30, mwaka 2017 kutokana na kudai kuwa chama hicho kinaenda kinyume na miiko yake.
Tangu ajiunge na Chadema, Nyalandu amekuwa kimya na mara chache amekuwa akijitokeza kwenye matukio ya chama hicho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *