MESSI bado anaiota Liverpool, hana raha na kiatu cha dhahabu

Mchezo wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya msimu huu wa 2018/19 kati ya Liverpool na FC Barcelona ulikuwa moja kati ya mechi za nusu fainali zilizotoa matokeo ambayo yaliwshangaza wengi sana kutokana na jinsi watu wengi walivyotabiri.

Na zaidi ni ule mchezo wa marudiano ambapo FC Barcelona walipewa nafasi kubwa ya kufuzu kutokana na kuwa na mtaji mzuri wa magoli katika ushindi ambao waliupata katika Uwanja wao wa nyumbani wa Camp Nou.

Katika mchezo wa awali miamba hiyo ya Nou Camp iliibuka na ushindi wa mabao 3-0, na safari yao ya Anfield ilikuwa nikwenda kutafuta sare au kutoruhusu zaidi ya magoli mawili.

Lakini jambo la kushangaza Barcelona walijikuta wakiruhusu mabao 4 kwa bila na moja kwa moja kutupwa nje ya michuano hiyo kwa wastani wa mabao 4-3 na kufuta ndoto ya Barcelona kuendelea na mbio za kuwania ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Moja ya watu walioumizwa kwa kiasi kikubwa na kipigo hicho ni nahodha wa Barcelona, Lionel Messi, ambaye amesema ameumizwa sana na kipigo hicho hadi kukosa raha ya ukifikiria kiatu cha dhahabu cha UEFA.

Alipoulizwa anajisikiaje kutwaa kiatu cha sita cha dhahabu cha michuano ya Ulaya akifunga magoli 12 tofauti ya magoli manne na wanaomfuatia, alijibu kuwa furaha yake haijakamilika kutokana na kuondolewa katika michuano hiyo na hafikiri tuzo binafsi.

“Kiukweli sifikiri hata kidogo kiatu cha dhahabu cha michuano ya Ulaya, hakipo akilini mwangu kabisa kilichotokea Liverpool ndio kilichopo kichwani kwangu,” Messi amesema.

Hata hivyo fainali ya Champions League itakayozikutanisha timu za Liverpool na Tottenham June 1 2o19 katika jiji la Madrid nchini Uhispania, hakuna hata mchezaji mmoja ambaye anaweza kumfikia magoli Messi kutokana na wote kuwa na magoli machache.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *