Hatima ya Amissi Tambwe Yanga haijulikani

Mshambuliaji wa Yanga, Amissi Tambwe mpaka sasa hatima yake haijajulikana, hii ni kwa mujibu wa vyanzo vya karibu vya mchezaji huyo.
Taarifa zaidi zinaeleza kuwa Tambwe amesema kuwa mpaka sasa uamuzi wa yeye kuendelea kubaki klabuni hapo unabaki kwa kocha wake Mwinyi Zahera.
Pia imeelezwa kuwa Tambwe amesema mpaka sasa ana ofa tatu mezani ambapo moja inatoka kwao Burundi na nyingine Zambia na moja ni ya hapa hapa Tanzania.
Licha ya uwepo wa ofa hizo, Tambwe amesema bado anawapa Yanga kipaumbele cha kwanza kabla ya kufanya maamuzi mengine kwenda sehemu nyingine.


Tambwe ni miongoni mwa washambuliaji ambao wamewahi kutamba katika kufumania nyavu licha makali yako kupungua kutokana na kukosa nafasi ya kudumu katika kikosi cha kwanza kufuatia majeruhi ya mara kwa mara.
Tambwe alikuja Tanzania msimu wa 2013/14 ambapo akiwa Simba aliibuka mfungaji bora kwa kufikisha idadi ya mabao 19 ambapo baadaye aliibukia Yanga ambapo alimaliza na magoli 14.
Msimu wa 2015/16 Tambwe aliibuka tena mfungaji bora baada ya kufunga magoli 21 na msimu wa 2016/17 alifunga mabao 11.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *