Aliyekuwa mchezaji wa Harambee Stars apigwa marufuku na FIFA

Image result for george owino

Aliyekuwa mchezaji wa Harambee Stars George Owino ni mmoja wa watu tisa ambao uongozi wa kambumbu duniani FIFA imewapiga marufuku kwa shughuli zote zinazohusiana na kambumbu kwa muda wa miaka kumi.

Pamoja na marufuku, Owino pia alitozwa faini ya shillingi millioni moja nukta tano na FIFA kwa kukarabati mechi.

Kamati ya adabu ya FIFA ilipata kuwa watu tisa, nane ambao ni wachezaji / waliokuwa wachezaji na pia wakala wa mchezaji mmoja, walipatakana na hatia ya kujihusisha na kuendesha mechi ambayo ni ukiukaji wa makala ya 69 ya FIFA.

Wanaofuata ni watu ambao wamepigwa marufuku ya kujihusisha na shughuli zozote za michezo ndani na nje ya nchi kwa maisha yao yote.

Image result for george owino

Bw. Karlon Murray, Trinidad and Tobago
Bw. Keyeno Thomas, Trinidad and Tobago
Bw. Hellings Mwakasungula, Malawi
Bw. Ibrahim Kargbo, Sierra Leone
Bw. Kudzanai Shaba, Zimbabwe
Bw. Séïdath Tchomogo, Benin
Bw. Leonel Duarte, Cuba

Image result for george owino

Matukio haya ya kinidhamu kwa watu waliotajwa yalitokana na uchunguzi unaohusiana na mechi nyingi ambayo Bw. Wilson Raj Perumal alijaribu kuendesha mchezo wa kamari. Huu uchunguzi pana ulifanywa na FIFA kwa miaka nyingi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *