
Mwili wamerehumu Daktari Hamisi Juma umerejeaa nchini kutoka Cuba.
Daktari Juma inasemekana alijitoa Uhai Kupitia Masaibu aliyokuwa anapitia akiwa na wenzake.

Marehemu Juma ni mmoja kati ya madakitari 50 waliosafiri nchini kuongeza ujuzi kupitia mpango wa serikali baina ya Kenya na Cuba.
Hapo jana kamati ya bunge kuhusu iliwaita maafisa kutoka wizara ya afya nchini, kuelezea jinsi serikali inavyoshughulikia changamoto zinazowakumba madaktari wa Kenya waliomo nchini CUBA.

Akijibu masuali ya wabunge katibu katika wizara ya afya Susan Mochache, ameitetea serikali akisema madakitari walioenda nchini CUBA hawakuwekewa vikwazo vya kurejea nchini, na kwamba walitengewa pesa za kutosha kuwawezesha kurudi nyumbani.




